Tuesday, 25 October 2011

Simba, Yanga nani zaidi Jumamosi?

Kocha wa Simba, Moses Basena
YANGA na Simba zinaingia kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumamosi Oktoba 29, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani.

Hata hivyo, tayari mashabiki wa Yanga wameanza 'minong'ono' hasa baada ya kocha wa sasa Sam Timbe kuondolewa na kuja kwa Kosta Papic kunaweza kuwavuruga wachezaji hasa kutokana na kila mmoja kuwa na mfumo wake wa uchezaji.

Simba vs Yanga
Mashabiki wa soka wanasema kuwa hiyo ni nafasi kwa Simba kutumia mwanya huo, lakini vilevile wapo wenye mtazamo tofauti wanaosema kuwa Simba wanaweza wakapigwa endapo watafikiria hayo na Yanga kutumia staili walioyoizoea ya Timbe.

Pamoja na hayo, Yanga ina kikosi ambacho zaidi wanamtegemea Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza lakini kwa upande wa Simba, vilevile watakuwa na Haruna Moshi 'Boban', Emmanuel Okwi na Felix Sunzu. Boban na Sunzu ndiyo walioiua Yanga katika Ngao ya Jamii ya ufunguzi wa Ligi Kuu.


Kocha wa Simba, Moses Basena amekwishasema kuwa hana wasiwasi na Yanga kwa kuwa anachukulia kama mechi nyingine ya ligi.

Wakenya wahofia gharama za maisha kupanda

WAKATI majeshi ya Kenya yakielekea mpakani mwa Kenya na Somalia, tayari wananchi wa Kenya wameanza kuingiwa na wasiwasi wa kupanda kwa gharama za maisha kwamba kazi sasa itakuwa kuendeleza fedha kwa mapambano dhidi ya Al-Shabaab.
Itamlazimu mfanyakazi kulipa Sh7,000 na Sh10,000 (kati ya dola 70 hadi 100) kila siku kwa ajili ya kumwezesha askari mmoja kuishi katika uwanja wa mapambano; hiyo ni sawa na Sh300,000 (dola 2,865) kwa mwezi au sawa na Sh3.6 million (dola 34, 285) kwa mwaka.
Hadi kufikia wiki iliyopita, Kenya ilikuwa imeondoa kodi na makato mengine kwa askari wa Kenya kwa ajili ya kufanya kazi kwa amani ya kulinda Wakenya.
Wakati majeshi yakielekea mpakani, walipakodi wameanza kukumbana na machungu ya kodi kubwa tangu uhuru, na kwamba wataalam wa masuala ya kiuchumi wamesema itakuwa juu.
Maofisa wa Usalama hawakuwa tayari kusema kiasi gani cha fedha jeshi litatumia katika muda wa mapambano haufahamiki na pia, mapambano ya jeshi huvuruga uchumi na bajeti za nchi.
“Pesa za vita, huwezi kuziweka katika bajeti ya maendeleo. Ni kama pesa za dharura. Kama hazitoshelezi, sasa ni wakati wa serikali kuangalia, miradi gani ya kuisimamisha na fedha kuelekezwa huku,” anasema Simiyu Werunga, machambuzi wa masuala ya usalama.
Serijkali inaingia katika vita ambayo haikupangiwa bajeti huku serikali ikikabiliwa na upungufu wa Sh236 billion kati ya Sh1.2 trilioni ya fedha za bajezi kama ilivyoelezwa na  Waziri wa Fedha, Uhuru Kenyatta mapema Juni.

Majeshi ya Kenya yasonga mpakani

Vikosi vya Jeshi la Kenya vikisonga mbele. Picha ya Daily Nation.
Majeshi ya Kenya yakienda Liboi, karibu na mpaka wa Somalia tayari kwa mapambano dhidi ya makundi ya waasi wa Somalia yakiongozwa na kikundi cha Al-Shabaab.
Tayari maguruneti mawili yameshalipuka katikati ya jiji la Nairobi na watu kadhaa kujeruhiwa huku ikiripotiwa mtu mmoja kufariki dunia.

Friday, 14 October 2011

Yanga yaishinda Kagera Ligi Kuu Bara

Muuaji wa Kagera Sugar,
Kenneth Asamoah.
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga, wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuilaza Kagera Sugar bao 1-0 katika mchezo kali ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa leo.

Yanga iliyokuwa nyuma ya hasimu wao Simba kwa pointi 10, imejivuta sana na kufikisha pointi 15 na kubakisha pointi tatu kuwafikia mahasimu wao. Simba itashuka dimbani Jumapili kucheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mechi hiyo, bao la Yanga lilifungwa na Kenneth Asamoah.

Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki ijayo

Mechi za Jumanne Okt. 18 2011
CSKA Moscow v Trabzonspor, Kundi B, 17:00
Dinamo Zagreb v Ajax, Kundi D, 19:45
FC Basel v Benfica, Kundi C, 19:45
Lille v Inter Milan, Kundi B, 19:45
Man City v Villarreal, Kundi A, 19:45
Napoli v Bayern Munich, Kundi A, 19:45
Real Madrid v Lyon, Kundi D, 19:45
SC Otelul Galati v Man Utd, Kundi C, 19:45

Jumatano, Okt. 19, 2011
AC Milan v BATE Borisov, Kundi H, 19:45
Barcelona v Plzen, Kundi H, 19:45
Bayer Leverkusen v Valencia, Kundi E, 19:45
Chelsea v Genk, Kundi E, 19:45
FC Porto v Apoel Nicosia, Kundi G, 19:45
Marseille v Arsenal, Kundi F, 19:45
Olympiakos v Borussia Dortmund, Kundi F, 19:45
Shakhtar Donetsk v Zenit St Petersburg, Kundi G, 19:45

Tuesday, 11 October 2011

Egypt crowned African champions to book a World Cup berth

Egypt's coach (sec. R) with his players after crowned the tittle.

Egypt was crowned African champions following their thrilling victory over giants Cameroon 3-1 (20-25, 25-28, 25-20, 25-22) in the final of the 2011 Men’s African Nations Championship held in Tangier, Morocco on Thursday.  Egypt secured a ticket to the 2011 FIVB World Cup set to take place in Japan from November 20 to December 4.

  The African champions will now move onto the Olympic qualifying event, with the top three from there earning a berth at the London 2012 Olympic Games.

 Egypt achieved an unpreceeded record of wining the title for the fourth in row and a total of 6 crowns, but they still behind Tunisia who has eight trophies under their name and deprived Cameroon from gaining their third cup

 Meanwhile Tunisia returned back to podium after being out two years ago when they were ranked fifth as they outlasted Algeria 3-1 (28-26, 19-25, 25-18, 25-22) in the bronze medal match.

 The final was attended by Tangier Governor Hassar, CAVB President Dr Amr Elwani, Morocco Volleyball Federation President Abdelhadi Ghzali, Local organizing committee president Lahcene Chater, CAVB Vice President Majore Timba and Board members Mory Keita and Hassan Ahmed as well as a lot of the local authorities.

Final Match
Egypt Beat Cameroon 3-1 (20-25, 25-28, 25-20, 25-22)
                                                                                
 Defending champions Egypt succeeded to keep the African title on their homelands after the down the struggling Cameroon team 3-1 (20-25, 25-28, 25-20, 25-22) in a fantastic final in front of 3000 Moroccan spectators most of them supported Egypt.

 “We didn’t expect this big support from the Moroccan spectators who made us fell as if we are playing at home,” Said Egypt coach Sherif El Shemerly happily after the match.
 “I’m very happy to achieve my first title with the senior national team after a lot of achievements with the youth and Junior teams and now we are looking forwards to represent Africa in the World Cup. I’m happy with the performance of all my players because most of them apply our a strategy against a strong team like Cameroon.” He added.

 Cameroon started the match as the better side when they used the spikes of Jean Ndaki from position 2 and Didier Sali in position 4 to lead 8-5 at the first TTO. Egytp team made a lot of reception and service mistakes that allowed Cameroon to stay ahead 16-12 in the first technical timeout. Although Egypt struggled to come back through the well known spike service of Ahmed Salah and Abdalla Abdel Salam, but Cameroon palyers became highly motivated to win the set and they made it 25-20.
 Egypt started the second set with organized line up and succeeded to come back 4-1 for Cameroon to lead for the first time 8-7 at the first TTO. Cameroon came back through the quick attacks of Zamgum Nongny and Sem Dolegombai to lead narrowly 16-15 at the second TTO. Mohamed Abdel Moneim and Saleh Fathy started working from position 4 with the combinations of their skilful setter Abdalla to win the set 25-18 after a group of mistakes form Cameroon team in spiking and receiving.
 Egypt continued their dominance through the service in the third set while Cameroon coach started to make some substitutions that disturb the unity of the team and Egypt succeeded to use this to win the set 25-20 after three aces from Salah.
 Cameroon emerged back in the fourth set to save the match and their big gun Ndaki hammered the Egyptians with his attacks to lead 8-7. The Egyptian team used the strategy of the quick attacks through the centers Abdel Latif Osman and Rashad Shebl to win the difficult set 25-22.  

Bronze Medal Match
Tunisia beat Algeria 3-1 (28-26, 19-25, 25-18, 25-22)
                                                      
 Tunisia won the critical points of each set in their way to see off Algeria 3-1 (28-26, 19-25, 25-18, 25-22) in the bronze medal encounter lasting 98 minutes. Tunisia achieved the bronze medal for the
 The match started with a tight competition between both teams with Algeria having the upper hand after leading 8-7 at the first TTO. The match went point by point with both teams deploying their block against the main attackers. Algeria opposite attacker Taoufik Mahdjoubi was prominent in his powerful attacks while his Tunisian counterpart Hichem Kaabi did a good job in his skilful attacks that made his team stay in draw till 20-20. Algeria led again 24-23 with Billel Soualem spikes, but Tunisia saved two set points before Tunisia won 28-26.
 The second set showed Algerian dominance through their better reception and they led 8-5 at the first TTO. The Tunisian team tried to come back through their experienced spiker Nooreddine Hfaied and Hamza Nagga, but Algeria again arranged their combinations using Mahdjoubi and Soualem to lead 16-11 at the second TTO before they continued their wide lead till they won the set 25-19 to draw 1-1.
 The third set again started competitive till the draw 5-5 when Tunisia emerged with the spikes of Kaabi and Ismail Moalla to lead 16-11 at the second TTO. Tunisia led the situation with their good reception to win the set 25-18.
 Algeria struggled to save the match as the coach made some substitutions fielding back the captain Ali Kerboua, but Tunisia were more motivated to win as they used the spike service of Nagga and Moalla to win several popints beside the fast attacks through the centers to win the set 25-22 and the match 3-1.

Individual Awards
  • Best Setter: Abdalla Abdel Salam (EGY)
  • Beast Libero: Rafik Djoudi (ALG)
  • Best Digger: Anwer Taouerghi (TUN)
  • Best Blocker: Sem Dolegombi (CMR)
  • Best Server: Ahmed Salah (EGY)
  • Best Spiker: Jean Ndaki (CMR)
  • Most Valuable Player MVP: Ahmed Salah (EGY)

Final Results

Final:
Cameroon v Egypt (20-25, 25-28, 25-20, 25-22) 
Bronze medal:
Tunisia v Algeria 3-1 (28-26, 19-25, 25-18, 25-22)
5-6 places:
Congo Brazzaville v Morocco 3-1 (25-23, 25-22, 18-25, 25-21)
7-8 places:
South Africa v Botswana 3-1 (25-23, 25-22, 21-25, 26-24)

 All Results and Ranking
Final ranking
  1. Egypt
  2. Cameroon
  3. Tunisia
  4. Algeria
  5. Congo Brazzaville
  6. Morocco
  7. South Africa
  8. Botswana

 

Kikapu kinaposhika kasi Indoor

Kantore Sandra (kushoto) wa timu ya kikapu ya Berco Stars ya Burundi  akijaribu kufunga huku 
Lucy Augustino wa Jeshi Stars akimtazama wakati wa Mashindano ya Klabu
Bingwa ya Kikapu Kanda ya Tano Afrika yanayoendelea kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini
Dar es Salaam. Picha ya Odoyo Jackson wa Mwananchi.

Chamudata ilivyomuunga mkono Msama


Mlezi wa Chama cha Wanamuziki wa Nyimbo za Injili, Martha Mlata
(kushoto) ambaye
pia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, akimkabidhi tuzo
Mkurugenzi wa Msama Promotions.

* Taasisi nyingine nazo zimuunge mkono
* Asomesha yatima 50, asaidia wajane 25
* Adhamiria kutoa vitanda hospitali Mtwara
* Sasa anamsubiri Lukuvi kumtafutia wafadhili

Mwandishi Maalum
"NINACHOWEZA kusema ni kwamba Kampuni ya Msama Promotions imedhamiria kutekeleza kwa vitendo jukumu kubwa la Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete la kupambana na ukosefu wa ajira, na tuko mstari wa mbele kuwasaidia watoto yatima."
Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions, Alex Msama anayebainisha kwamba kutokana na dhamira hiyo, ndiyo maana wamekuwa mstari wa mbele kuandaa matamasha ya muziki wa Injili, lengo likiwa ni kupata fedha kuchangia watoto yatima.
Kutokana na kuwa mstari wa mbele kudhibiti kazi za wasanii, Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania (Chamuta) kimeamua kumpa tuzo Msama. Heko Chamuta kwa kuthamani mchango wake, na kutoa changamoto kwa taasisi nyingine kuiga mfano huo.
Chamuta wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata waliandaa tafrija maalumu kwa ajili ya kumpongeza Msama kwa kutambua mchnago wake huku wakimkabidhi tuzo, ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wao kama wadau.
Msama amekuwa akitumia muda wake mwingi kupambana na maharamia wanarudufu kazi za wasanii, na kutokana na tuzo aliyopewa, anasema ndio kwanza mapambano yameanza, kwani ameahidi kuongeza kasi zaidi akishirikiana na Jeshi la Polisi nchini na taasisi nyingine husika.
Mlata alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuunga mkono jitihada za Msama, ikiwa ni pamoja na Watanzania wengine kwa ujumla.
Akizungumzia mambo mengine zaidi, Msama anasema mapato yanayotokana na matamasha mbalimbali ikiwa ni pamoja na la Pasaka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kiasi yalitumika kuchangia wajane 25 wasiojiweza na kusomesha watoto yatima katika mikoa ya Dodoma, Tabora na Shinyanga.
Msama anasema huo ndio utaratibu wao, fedha wanazopata wamekuwa wakitumia kusomesha yatima na kuwatafutia ajira mbalimbali wasiojiweza ikiwa ni pamoja na wengine kupata mafunzo ya kunadi vitu kupitia kampuni yake ya Msama Auction Mart.
Mkurugenzi huyo anasema mpaka sasa wanasomesha wanafunzi takriban 50 katika shule mbalimbali Dar es Salaam zikiwamo St. Mary's, George Washington, VETA, Lugalo, Colnelius na Biafra.
Anasema pia wamekuwa wakitoa semina za kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kufanya biashara na kuachana na dawa za kulevya.
Msama Promotions pia ilikamilisha ahadi yake ya kuwasaidia wanawake wajane fedha za mitaji ya biashara kwa kuwakabidhi wajane 25 fedha taslimu sh. 150,000 kila mmoja, jumla ikiwa ni sh. milioni 4.
Msama anasema alitimiza ahadi aliyoitoa wakati wa maandalizi ya tamasha la Pasaka lililofanyika Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee huku mgeni rasmi akiwa Rais Kikwete.
Msama anasema fedha hizo zilipatikana kutokana na mauzo ya albamu ya Haleluya Collection Vol 5 iliyozinduliwa katika tamasha la Pasaka.
Wanawake hao wajane waliokabidhiwa fedha hizo za mitaji wametoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Pia fedha zilizopatikana kwenye tamasha hilo zinatumika kusaidia kuwasomesha watoto yatima mikoa ya Tabora, Dodoma na Shinyanga kwa awamu hii.
Msama Promotions tayari imeshatoa msaada wa sh. milioni 3 kwa waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Vitu vilivyotolewa ni magunia manne ya mchele, kila moja likiwa na kilo 120, magunia mawili ya maharage, magunia 10 ya unga wa mahindi, mifuko miwili ya sukari, mifuko mitatu ya unga wa ngano yenye kilo 25 kila moja na ndoo mbili za mafuta ya kupikia.
"Lengo kubwa la tamasha la Pasaka linaloratibiwa na Msama Promotions ni kusaidia watoto yatima na jamii kwa ujumla... ndio maana hata  walioathirika kwa kwa mabomu tuliwasaidia," anasema Msama.
Akipokea msaada huo, mtangazaji wa Clouds FM, Anthonio Nugazi anayeendesha kipindi cha Kambi Popote, alimshukuru Msama kwa kuonesha moyo wa kujitolea, na akatoa mwito kwa Watanzania wengine kuiga mfano.
Tamasha la Pasaka la nyimbo za Injili za kumsifu Mungu, lilifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Apili 24 mwaka huu, Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kushirikisha wasanii kutoka nchi za Kenya, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Akisoma risala mbele ya Rais Kikwete kuhusu tamasha hilo ambalo mwaka huu liliadhimisha jubilee ya miaka 10 tangu kuanzishwa, Askofu wa Kanisa la TAG, Lawrence Kameta alimuomba Rais Kikwete kuwashauri viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupunguza gharama za vibali vya kuwaalika wasanii wa nje kwa ajili ya tamasha hilo.
Alisema kwa vile tamasha hilo limelenga kusaidia watu wasiojiweza, wajane na walemavu na kwamba si tamasha la kibiashara, ipo haja ya BASATA kupunguza gharama hizo ili miaka ijayo liwe na waimbaji wengi kutoka nje ya nchi ikiwa ni moja ya njia ya kudumisha umoja kati ya Tanzania na nchi jirani.
Ombi jingine lililotolewa na kampuni hiyo kwa Rais Kikwete ni kupewa eneo la ardhi itakayojengwa ili makundi ya watu wasiojiweza wakutane katika eneo hilo na kupata msaada wa mahitaji yao.
Pia waliomba Serikali kusaidia kushawishi kampuni za vinywaji baridi na za simu kuunga mkono kufadhili tamasha hilo kwani hufikia kubaki na madeni baada ya tamasha kumalizika.
Akijibu ombi hilo, Rais Kikwete aliwaeleza BASATA kutekeleza ombi hilo kwani kazi inayofanywa na Msama Promotions ya kusaidia makundi ya watu wasiojiweza ni kubwa na linapojitokeza tatizo la kuhitaji msaada wa kulifanikisha, Serikali inatakiwa kuonesha msaada wake.
Kazi ya kutafuta wafadhili na kuchangisha, Rais Kikwete alimkabidhi Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera na Bunge, William Lukuvi kwa vile anaimudu.
Wasanii wa nyimbo za injili wakiimba wimbo maalumu wa
 kutimiza miaka 50 ya Uhuru