Tuesday, 25 October 2011

Wakenya wahofia gharama za maisha kupanda

WAKATI majeshi ya Kenya yakielekea mpakani mwa Kenya na Somalia, tayari wananchi wa Kenya wameanza kuingiwa na wasiwasi wa kupanda kwa gharama za maisha kwamba kazi sasa itakuwa kuendeleza fedha kwa mapambano dhidi ya Al-Shabaab.
Itamlazimu mfanyakazi kulipa Sh7,000 na Sh10,000 (kati ya dola 70 hadi 100) kila siku kwa ajili ya kumwezesha askari mmoja kuishi katika uwanja wa mapambano; hiyo ni sawa na Sh300,000 (dola 2,865) kwa mwezi au sawa na Sh3.6 million (dola 34, 285) kwa mwaka.
Hadi kufikia wiki iliyopita, Kenya ilikuwa imeondoa kodi na makato mengine kwa askari wa Kenya kwa ajili ya kufanya kazi kwa amani ya kulinda Wakenya.
Wakati majeshi yakielekea mpakani, walipakodi wameanza kukumbana na machungu ya kodi kubwa tangu uhuru, na kwamba wataalam wa masuala ya kiuchumi wamesema itakuwa juu.
Maofisa wa Usalama hawakuwa tayari kusema kiasi gani cha fedha jeshi litatumia katika muda wa mapambano haufahamiki na pia, mapambano ya jeshi huvuruga uchumi na bajeti za nchi.
“Pesa za vita, huwezi kuziweka katika bajeti ya maendeleo. Ni kama pesa za dharura. Kama hazitoshelezi, sasa ni wakati wa serikali kuangalia, miradi gani ya kuisimamisha na fedha kuelekezwa huku,” anasema Simiyu Werunga, machambuzi wa masuala ya usalama.
Serijkali inaingia katika vita ambayo haikupangiwa bajeti huku serikali ikikabiliwa na upungufu wa Sh236 billion kati ya Sh1.2 trilioni ya fedha za bajezi kama ilivyoelezwa na  Waziri wa Fedha, Uhuru Kenyatta mapema Juni.

No comments:

Post a Comment