Kocha wa Simba, Moses Basena |
YANGA na Simba zinaingia kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumamosi Oktoba 29, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani.
Hata hivyo, tayari mashabiki wa Yanga wameanza 'minong'ono' hasa baada ya kocha wa sasa Sam Timbe kuondolewa na kuja kwa Kosta Papic kunaweza kuwavuruga wachezaji hasa kutokana na kila mmoja kuwa na mfumo wake wa uchezaji.
Simba vs Yanga |
Mashabiki wa soka wanasema kuwa hiyo ni nafasi kwa Simba kutumia mwanya huo, lakini vilevile wapo wenye mtazamo tofauti wanaosema kuwa Simba wanaweza wakapigwa endapo watafikiria hayo na Yanga kutumia staili walioyoizoea ya Timbe.
Pamoja na hayo, Yanga ina kikosi ambacho zaidi wanamtegemea Kenneth Asamoah na Hamis Kiiza lakini kwa upande wa Simba, vilevile watakuwa na Haruna Moshi 'Boban', Emmanuel Okwi na Felix Sunzu. Boban na Sunzu ndiyo walioiua Yanga katika Ngao ya Jamii ya ufunguzi wa Ligi Kuu.
Kocha wa Simba, Moses Basena amekwishasema kuwa hana wasiwasi na Yanga kwa kuwa anachukulia kama mechi nyingine ya ligi.
No comments:
Post a Comment