Mlezi wa Chama cha Wanamuziki wa Nyimbo za Injili, Martha Mlata (kushoto) ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Msama Promotions. |
* Taasisi nyingine nazo zimuunge mkono
* Asomesha yatima 50, asaidia wajane 25
* Adhamiria kutoa vitanda hospitali Mtwara
* Sasa anamsubiri Lukuvi kumtafutia wafadhili
Mwandishi Maalum
"NINACHOWEZA kusema ni kwamba Kampuni ya Msama Promotions imedhamiria kutekeleza kwa vitendo jukumu kubwa la Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete la kupambana na ukosefu wa ajira, na tuko mstari wa mbele kuwasaidia watoto yatima."
Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions, Alex Msama anayebainisha kwamba kutokana na dhamira hiyo, ndiyo maana wamekuwa mstari wa mbele kuandaa matamasha ya muziki wa Injili, lengo likiwa ni kupata fedha kuchangia watoto yatima.
Kutokana na kuwa mstari wa mbele kudhibiti kazi za wasanii, Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania (Chamuta) kimeamua kumpa tuzo Msama. Heko Chamuta kwa kuthamani mchango wake, na kutoa changamoto kwa taasisi nyingine kuiga mfano huo.
Chamuta wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata waliandaa tafrija maalumu kwa ajili ya kumpongeza Msama kwa kutambua mchnago wake huku wakimkabidhi tuzo, ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wao kama wadau.
Msama amekuwa akitumia muda wake mwingi kupambana na maharamia wanarudufu kazi za wasanii, na kutokana na tuzo aliyopewa, anasema ndio kwanza mapambano yameanza, kwani ameahidi kuongeza kasi zaidi akishirikiana na Jeshi la Polisi nchini na taasisi nyingine husika.
Mlata alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuunga mkono jitihada za Msama, ikiwa ni pamoja na Watanzania wengine kwa ujumla.
Akizungumzia mambo mengine zaidi, Msama anasema mapato yanayotokana na matamasha mbalimbali ikiwa ni pamoja na la Pasaka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kiasi yalitumika kuchangia wajane 25 wasiojiweza na kusomesha watoto yatima katika mikoa ya Dodoma, Tabora na Shinyanga.
Msama anasema huo ndio utaratibu wao, fedha wanazopata wamekuwa wakitumia kusomesha yatima na kuwatafutia ajira mbalimbali wasiojiweza ikiwa ni pamoja na wengine kupata mafunzo ya kunadi vitu kupitia kampuni yake ya Msama Auction Mart.
Mkurugenzi huyo anasema mpaka sasa wanasomesha wanafunzi takriban 50 katika shule mbalimbali Dar es Salaam zikiwamo St. Mary's, George Washington, VETA, Lugalo, Colnelius na Biafra.
Anasema pia wamekuwa wakitoa semina za kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kufanya biashara na kuachana na dawa za kulevya.
Msama Promotions pia ilikamilisha ahadi yake ya kuwasaidia wanawake wajane fedha za mitaji ya biashara kwa kuwakabidhi wajane 25 fedha taslimu sh. 150,000 kila mmoja, jumla ikiwa ni sh. milioni 4.
Msama anasema alitimiza ahadi aliyoitoa wakati wa maandalizi ya tamasha la Pasaka lililofanyika Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee huku mgeni rasmi akiwa Rais Kikwete.
Msama anasema fedha hizo zilipatikana kutokana na mauzo ya albamu ya Haleluya Collection Vol 5 iliyozinduliwa katika tamasha la Pasaka.
Wanawake hao wajane waliokabidhiwa fedha hizo za mitaji wametoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Pia fedha zilizopatikana kwenye tamasha hilo zinatumika kusaidia kuwasomesha watoto yatima mikoa ya Tabora, Dodoma na Shinyanga kwa awamu hii.
Msama Promotions tayari imeshatoa msaada wa sh. milioni 3 kwa waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Vitu vilivyotolewa ni magunia manne ya mchele, kila moja likiwa na kilo 120, magunia mawili ya maharage, magunia 10 ya unga wa mahindi, mifuko miwili ya sukari, mifuko mitatu ya unga wa ngano yenye kilo 25 kila moja na ndoo mbili za mafuta ya kupikia.
"Lengo kubwa la tamasha la Pasaka linaloratibiwa na Msama Promotions ni kusaidia watoto yatima na jamii kwa ujumla... ndio maana hata walioathirika kwa kwa mabomu tuliwasaidia," anasema Msama.
Akipokea msaada huo, mtangazaji wa Clouds FM, Anthonio Nugazi anayeendesha kipindi cha Kambi Popote, alimshukuru Msama kwa kuonesha moyo wa kujitolea, na akatoa mwito kwa Watanzania wengine kuiga mfano.
Tamasha la Pasaka la nyimbo za Injili za kumsifu Mungu, lilifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Apili 24 mwaka huu, Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kushirikisha wasanii kutoka nchi za Kenya, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Akisoma risala mbele ya Rais Kikwete kuhusu tamasha hilo ambalo mwaka huu liliadhimisha jubilee ya miaka 10 tangu kuanzishwa, Askofu wa Kanisa la TAG, Lawrence Kameta alimuomba Rais Kikwete kuwashauri viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupunguza gharama za vibali vya kuwaalika wasanii wa nje kwa ajili ya tamasha hilo.
Alisema kwa vile tamasha hilo limelenga kusaidia watu wasiojiweza, wajane na walemavu na kwamba si tamasha la kibiashara, ipo haja ya BASATA kupunguza gharama hizo ili miaka ijayo liwe na waimbaji wengi kutoka nje ya nchi ikiwa ni moja ya njia ya kudumisha umoja kati ya Tanzania na nchi jirani.
Ombi jingine lililotolewa na kampuni hiyo kwa Rais Kikwete ni kupewa eneo la ardhi itakayojengwa ili makundi ya watu wasiojiweza wakutane katika eneo hilo na kupata msaada wa mahitaji yao.
Pia waliomba Serikali kusaidia kushawishi kampuni za vinywaji baridi na za simu kuunga mkono kufadhili tamasha hilo kwani hufikia kubaki na madeni baada ya tamasha kumalizika.
Akijibu ombi hilo, Rais Kikwete aliwaeleza BASATA kutekeleza ombi hilo kwani kazi inayofanywa na Msama Promotions ya kusaidia makundi ya watu wasiojiweza ni kubwa na linapojitokeza tatizo la kuhitaji msaada wa kulifanikisha, Serikali inatakiwa kuonesha msaada wake.
Kazi ya kutafuta wafadhili na kuchangisha, Rais Kikwete alimkabidhi Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu, Sera na Bunge, William Lukuvi kwa vile anaimudu.

![]() |
Wasanii wa nyimbo za injili wakiimba wimbo maalumu wa kutimiza miaka 50 ya Uhuru |
No comments:
Post a Comment