Friday, 30 September 2011

Dewji: Siafiki Angetile kumtetea Poulsen


Na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARA na mwanamichezo maarufu nchini, Azim Dewji amesema kuwa, kamwe haafikiani na utetezi unaotolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetileh Osiah anayedai Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen hawezi kufukuzwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili.

Dewji aliyewahi kuifadhili Simba na kuipa mafanikio makubwa Afrika, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, wadau wana nafasi kubwa katika ustawi wa soka ya Tanzania, hivyo wasipuuzwe kwa majibu ya juu juu.

Alisema: “Nimesoma taarifa inayomnukuu Katibu Mkuu wa TFF kwamba Paulsen hawezi kutimuliwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili, tena kwa sababu ya maoni ya wadau.

“Binafsi nasema hii si sahihi. Kocha anapimwa kwa vigezo vingi, lakini kama ameshindwa kazi na haoneshi dalili za kuelekea kufanikiwa, kwanini aendelee kuachwa kazini? Nahisi Angetile amepotoka na kamwe siafiki utetezi wake.”

Dewji aliongeza kuwa, kocha huyo raia wa Denmark alipaswa kuifanyia mapinduzi ya soka Stars, lakini anashangazwa kuona kila kukicha akifanya sawa na waliomtangulia, kuita kikosi kwa ajili ya mechi fulani huku akiwatumia wachezaji `wazee’ badala ya kuibua na kuelea vipaji vipya kwa ustawi wa soka katika miaka ijayo.

Angetile Osiah
“Hakuna jipya na wadau wanakata tamaa, ndiyo maana wanatoa ushauri kwa sababu wanaipenda timu yao. Wakiendelea kukatishwa tamaa, nani atakwenda uwanjani na TFF itapata wapi fedha? Ni vyema wakalitafakari hili, kwani tunashuhudua makocha wenye mikataba wakiachishwa kazi baada ya kushindwa kukata kiu ya waajiri wao,” alisema Dewji.

Osiah, jana alikaririwa na vyombo vya habari akimtetea Poulsen baada ya wadau mbalimbali wa michezo nchini kuhoji uhalali wa kocha huyo kuendelea kutafuta fedha za Watanzania, ilhali haoneshi mwelekeo wowote, zaidi ya kuporomosha kiwango cha wachezaji wa Taifa Stars.

Miongoni mwa wadau hao ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu aliyeonesha hofu ya Tanzania kutonufaika na lolote kutoka kwa kocha Poulsen.

Akizungumza na waandishi wa habari za michezo juzi, Osiah alisema: “Tunaheshimu maoni ya wadau wetu, akiwamo Mbunge Mangungu (Murtaza), ila lazima tuelewe kuwa Poulsen yupo kisheria na mkataba wake ni wa miaka miwili, hivyo hatuwezi kumuacha kwa mtindo wanaoutaka wao.

Poulsen aliyetua nchini kuirithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo mwaka 2010, hajapata mafanikio makubwa akiwa na kikosi cha Stars, ukiondoa `ngekewa’ ya kutwaa Kombe la Challenge, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994. Ilishindwa kwa `matuta’ kuanzia hatua ya makundi hadi fainali.

Na hata baada ya kuingia katika michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2012 na ile ya Kombe la Dunia mwaka 2014, Stars imeendelea kuwa ile ile ya kubahatisha uwanjani, hali inayompa wakati mgumu Poulsen aliyewabwaga wenzake watano katika mchujo wa mwisho wa kundi la makocha 59 waliokuwa wameomba kumrithi Maximo.


Thursday, 29 September 2011

Matokeo Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi zilizochezwa jana usiku

Arsenal wakishangilia bao....
Kundi E
Valencia 1 Chelsea 1
Bayer Leverkusen 2 Racing Genk 0

Kundi F
Olympique Marseille 3 Borussia Dortmund 0
Arsenal 2 Olympiakos Piraeus 1

Kundi G
Shakhtar Donetsk 1 APOEL Nicosia 1
Zenit St Petersburg 3 Porto 1

Kundi H
AC Milan 2 Viktoria Plzen 0
BATE Borisov 0 Barcelona 5

Wednesday, 28 September 2011

...Mashabiki wa Michael Jackson

Mashabiki wa Michael Jackson nje ya mahakama...
Kaka wa Michael Jackson, Jermaine...

Wanandugu wa Michael Jackson wakienda mahakamani kusikiliza kesi ya daktari wa MJ

Wazazi wa Michael Jackson...
Janet Jackson naye akiingia mahakamani..

Mancini amtimua Tevez Man. City

Carlos Tevez akiitumikia klabu yake.
LONDON, England
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema anataka kuona Carlos Tevez "anajiondoa mwenyewe klabuni" baada ya kugoma kuingia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich.
Mancini alimtaka mchezaji huyo kuingia dakika 35 wakati timu yake ilipokuwa nyuma kwa mabao 2-0.
Mancini alisema: "Kama mimi ni kocha hapa, sitaki kumuona. Ameshamalizana na mimi.
"Kama tunataka kuimarisha timu, kwa mtu kama Carlos hatufai. Kwangu tumemalizana."

Man. United chupuchupu, Real yaua

LONDON, EnglandManchester United ilinusurika kuumbuka kwenye Uwanja wake wa Old Trafford baada ya kupata bao dakika ya 90 lililofungwa kwa kichwa na Ashley Young na kufanya matokeo kuwa 3-3 dhidi ya Basel katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Kundi C. Mabingwa hao wa Uswisi waliokuwa nyuma kwa mabao 2-0 walisawazisha na kufunga lingine na kufanya matokeo kusomeka 3-2.
United walionekana kuridhika na mabao mawili ya kipindi cha kwanza ya Danny Welbeck, lakini Basel ilisawazisha kabla ya Fabian Frei kufunga la tatu baada ya mabao ya Alexander Frei.
Wakati ndugu zao wakisalimika, Manchester City walitandikwa mabao 2-0 na Bayern Munich huku Mario Gomez akifunga mabao yote mawili katika mechi hiyo ya Kundi A na kuifanya Bayern kuwa na pointi sita katika mechi mbili.
Real Madrid, kwa upande wake, ilikuwa ikisaka rekodi ya taji la 10 la Ulaya kwa kujipatia pointi sita katika mechi ya Kundi D baada ya kuizabua 3-0  Ajax Amsterdam kwa mabao ya Cristiano Ronaldo, Kaka na Karim Benzema.
Inter Milan iliyokuwa nyuma kwa mabao 2-0 mbele ya CSKA Moscow iliibuka na kushinda mabao 3-2 baada ya kazi nzuri ya Mauro Zarate aliyefunga bao la ushindi na kufanya kikosi cha kocha, Claudio Ranieri kuendelea kujipa matumaini ya kufanya vizuri.
Mechi nyingine, Napoli iliifunga Villarreal 2-0 mechi ya Kundi A, Trabzonspor ikatoka sare ya 1-1 na Lille ikiwa ni mechi ya Kundi B wakati Benfica iliifunga Otelul Galati 1-0 katika Kundi C. Nayo Olympique Lyon ikailaza Dinamo Zagreb 2-0 katika mpambano wa Kundi D.

Mechi za Makundi E-H zinazochezwa leo Jumatano Sept. 28, 2011

Zenit St Petersburg v FC Porto
AC Milan  v Plzen
Arsenal  v Olympiakos
BATE Borisov v Barcelona
Bayer Leverkusen v Genk
Marseille  v Borussia Dortmund
Shakhtar Donetsk v Apoel Nicosia
Valencia  v Chelsea

Tuesday, 27 September 2011

Jackson's doctor Murray goes on trial

Michael Jackson's personal physician, Conrad Murray, has gone on trial in Los Angeles, charged with involuntary manslaughter of the singer.
Prosecutors say he acted with "gross negligence" and gave Jackson a lethal dose of the sedative propofol, on the night he died in June 2009.
The defence says Jackson gave himself too much of the drug, a sleeping aid.
If convicted, Dr Murray, 58, could face four years in jail and the loss of his medical licence.
Slurred recording
In Tuesday's opening statement, lead prosecutor David Walgren told the court the evidence would show "Conrad Murray repeatedly acted with gross negligence, repeatedly denied appropriate care to his patient, Michael Jackson".
Lead prosecutor, David Walgren, plays an audio recording said to be from Dr Conrad Murray's mobile phone
"That misplaced trust... cost Michael Jackson his life."
The court heard a recording of Jackson slurring while talking about planned comeback concerts.
Mr Walgren said the audio, aired in public for the first time, had come from Dr Murray's mobile phone.
"When people leave my show, I want them to say, 'I've never seen nothing like this in my life'," says the voice on the audio.
The prosecutor said Jackson's difficulty in speaking on the recording showed that Dr Murray ought to have realised the star should not have taken any more propofol.
Mr Walgren said that after administering a dose of the drug on the date of Jackson's death, Dr Murray had not been attentive to the star's health.
'Abandoned'
The prosecutor said the doctor had left to go to the bathroom and checked his mobile phone.
 
Chief prosecutor David Walgren: Michael Jackson trusted his life to the medical skills of Conrad Murray
"He [Murray] left him [Jackson] there, abandoned him to fend for himself," the prosecutor said.
Mr Walgren said when Dr Murray found Jackson unconscious, he did not immediately call the emergency services, instead telling a bodyguard to do so 20 minutes later.
Dr Murray also did not mention to paramedics or emergency room doctors that he had administered propofol, according to the prosecutor.
Hundreds of Jackson fans gathered outside court as the trial began with opening statements from defence and prosecution. The proceedings are being televised and broadcast online.
Jackson choreographer Kenny Ortega was set to be the first prosecution witnesses to take the stand.
Mr Ortega was expected to lead the court through some footage from Jackson's final rehearsals as the 50-year-old star prepared for his series of comeback concerts.
That video eventually became part of a documentary, This Is It, directed by Mr Ortega.
A judge has blocked some details of Jackson and Dr Murray's lives being discussed at the trial.
Extra dose?
Jackson's history with drugs and financial troubles, as well as Dr Murray's debts and personal affairs, will not come out in court.
Both sides were expected to focus on Jackson's last hours.
Multiple witnesses, including security guards, paramedics and emergency room doctors are to be called.
The prosecution also plans to play a recording of Dr Murray's police interview two days after Jackson's death, in which the doctor says he gave the singer propofol for his insomnia.
The disclosure led to charges being brought against Dr Murray in February 2010.
Propofol is usually administered intravenously, often during surgery.
Medical experts are expected to testify about the sedative's effects, as well as how a trace amount of the drug was found in Jackson's stomach.
Defence lawyers are putting forward the theory that Jackson drank or somehow administered an extra dose of propofol after Dr Murray left.
The trial is expected to last about five weeks.
The jury comprises seven men and five women, one African American, six whites and five Latinos.
BBC News

R.I.P. Wangari Maathai

President Barack Obama (Left) and his wife Michelle (Right) and Prof Wangari Maathai (Centre) during an AIDS awareness campaign in Nairobi, Kenya, in 2006. Photo by DailyNation.

Poulsen aita 23 kuikabili Morocco

Dua kabla ya mchezo



Release No. 98

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Septemba 27, 2011
 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco.
Kikosi hicho kitaingia kambini Septemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na kinatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu kwenye mji wa Marrakech.
 Wachezaji walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).
 Viungo wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam).
 Washambuliaji ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).    
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari - TFF

 

Dr Murray faces jury over Jacko death

LOS ANGELES, USA
More than two years after Michael Jackson's sudden death, the singer's personal physician is to stand trial on Tuesday. Dr Conrad Murray, 58, has pleaded not guilty to a charge of involuntary manslaughter. If convicted, the maximum sentence is four years in prison.
It was a hot midsummer day in Los Angeles on 25 June, 2009. Hollywood was mourning the loss of the actress Farrah Fawcett, as fans and celebrities paid tribute to the TV star, who had died from cancer, aged 62.
But that day will be remembered for another, altogether unexpected death and for the extraordinary outpouring of grief it provoked.
Pop star Michael Jackson, a month shy of his 51st birthday, was rushed to hospital and pronounced dead, his brother Jermaine confirming the news to stunned fans in a hastily-arranged press conference.
Jackson had recently stepped back into the limelight. He was rehearsing at the Staples Centre arena in Los Angeles for This Is It, his hugely anticipated concert series, which was due to start at the O2 in London on 13 July.
The night before his death, he worked until after midnight. The next day, shortly after noon, he was discovered unconscious in his bedroom by his physician Dr Conrad Murray.Dr Conrad Murray faces up to four years in prison if convicted
What happened in the time between those two events remains a mystery.
At a preliminary hearing, several witnesses gave detailed accounts of the frenzied activity at Jackson's home after the singer was found to be unresponsive.
The singer's death, according to the Los Angeles County Coroner, was a homicide caused by "acute Propofol intoxication." Propofol is a sedative that is normally used in hospitals to induce or maintain anaesthesia during surgical procedures.
But it will be up to a jury to decide whether the actions of Dr Murray, during the frantic efforts to revive the singer and in the hours before, caused his death.
BBC News

Persie aendelea kuiwekea 'pozi' Arsenal


Robie van Persie (katikati) wa Arsenal akiwa chini ya ulinzi wa wachezaji wa Newcastle katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya England. Persie ameendelea kuidengulia Arsenal baada ya kukaririwa leo akisema hajaamua kama ataitumikia klabu hiyo ya Emirates kwa muda mrefu.


Vumbi Ligi ya Mabingwa Ulaya leo

C. Ronaldo, Real Madrid
Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaingia hatua nyingine leo, baada ya timu kadhaa kufanya vema katika mechi za ufunguzi.
Manchester United, Manchester City na Inter Milan zina kazi ngumu leo kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Kila mmoja anatambua kuwa hakuna timu iliyotwaa ubingwa mara mbili tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, kila mmoja anaangalia jinsi gani ya kuivua ubingwa Barcelona.
Klabu hiyo ya Catalan itataka kujiimarisha zaidi kwani yenyewe na United zilitoka sare. Man United ilitoka sare na Benfica, City ilifanya hivyo kwa Napoli lakini Inter ilishangaza wengi kwa kuchapwa na Trabzonspor ikiwa nyumbani.
City, na United ambazo ziko kileleni mwa Ligi Kuu ya England, ilicheza na Napoli, na kuwalazimisha sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Etihad na kumwacha kocha, Roberto Mancini akijisifu "Nilichanganyikiwa kwa sababu ilikuwa mechi ya kwanza".
Mechi za leo
Bayern itakuwa na kazi ya kupunguza makali ya washambuliaji wa City wanaojengwa na Tevez, Balotelli, Owen Hargreaves na Yaya Toure.

W. Rooney, Man United

Hata hivyo, Bayern inajivunia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Villarreal na ushindi wake leo utaisaidia kujiweka katika nafasi nzuri zaidi.
Nayo Manchester United, kwa upande wake itakuwa na kibarua cha vijana wa Uswisi; Basel lakini watamkosa, Wayne Rooney.
Kocha wa United; Sir Alex Ferguson ameanza kuingia hofu kukosekana kwa Rooney, huku akiendelea kusikilizia maumivu ya Javier Hernandez aliyeumia katika mechi waliyotoka sare ya 1-1 na Stoke.
Naye kocha wa Basel, Thorsten Fink anasema ana kila sababu ya kuisimamisha United, kama alivyofanya kwa Bayern Munich ilipofungwa 1999 na Red Devils mechi ya Barcelona.
Inter ambayo ilianza vibaya ligi hiyo na baada ya kumtimua kocha wake, Giun Piero Gasperini na wamemnasa kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus, Claudio Ranieri.
Ranieri alishinda mechi ya kwanza 3-1 dhidi ya Bologna Jumamosi, lakini Wesley Sneijder, beki wa Brazil, Maicon na  kiungo wa Serbia, Dejan Stankovic watakosa mechi ya Kundi B, itakutana na CSKA mjini Moscow.
Katika kundi hilo, mabingwa wa Ufaransa, Lille itakutana na Trabzonspor wakati Lyon itacheza na Dinamo Zagreb, na Real Madrid itakuwa nyumbani kuivaa Ajax.

Adebayor: Nilicheza jicho moja sioni

Adebayor kushoto. PHOTO/Getty.
LONDON, England
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, ambaye aliingia kipindi cha pili katika mechi dhidi ya Wigan alicheza huku akiwa haoni jicho moja baadaya kugongana na mchezaji wa upinzani, lakini akasema anataka kuwa fiti ili aweze kufunga bao la kwanza dhidi ya Arsenal kufuta bao lile alilolaumiwa kwa kushangilia sana dhidi ya Arsenal alipokuwa akiitumikia Manchester City miaka miwili iliyopita."Sikuwa nauona mpira. Sikuwa naona mtu anayekuja," anasema Adebayor, ambaye hata hivyo, alicheza mechi hiyo hadi mwisho. "Lakini nzuri zaidi, nilikuwa na jicho moja, lakini tuliondoka na pointi tatu.Kipindi cha kwanza nilicheza vizuri kwa sababu nilikuwa naona kwa macho yote."

Keyshia, Gibson kufunga ndoa ya kufuru

HAWAII, Marekani
NYOTA wa R&B, Keyshia Cole amerudia kuzungumzia mipango ya sherehe za harusi yake itakayofanyika kwenye kitongoji cha Hawaii. Aliyasema hayo katika kipindi chake; TV show.
Keyshia, 29, anasema....nilikuwa na nyota wa kikapu wa Cleveland Cavaliers, Daniel Gibson wikiend na akaniambia maneno matamu baada ya kugombana miezi minne iliyopita.
Nyota huyo aliwaambia pia mashabiki wake, "Anataka tufunge ndoa ya 'kufuru' na anaandaa utaratibu wa kuleta wazazi wake hapa. Amenipa kitu 'baab kubwa' siwezi kusahau...ananipenda! Nimefurahi sana!"
Sherehe za harusi hiyo zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia kipindi cha Cole's reality TV show cha Family First, kinachoanza mapema February.
Mwanamuziki huyo kwa sasa ana watoto wawili, Daniel, mwenye miezi (10), na Gibson. Wawili hao walioana katika hafla ndogo iliyofanyika Cleveland, Ohio mapema Mei 11.

Monday, 26 September 2011

Berbatov could make a European return for Man. United

Berbatov
LONDON, England
IT is almost three years since his last Champions League goal and his mantle as fourth-choice striker is under threat from Michael Owen, yet Sir Alex Ferguson has denied he needs to repair Dimitar Berbatov's confidence ahead of Manchester United's encounter with Basel.
Berbatov has been frequently overlooked on the big occasions by Ferguson, notably the Champions League final defeat to Barcelona at Wembley in May, and may be required for United's opening home game in Europe this season. Wayne Rooney is a confirmed absentee with a hamstring injury, a problem with potential repercussions for England's Euro 2012 qualifier in Montenegro on Friday week, so too Javier Hernández with a dead leg he sustained at Stoke City on Saturday. With Danny Welbeck also easing his way back from a hamstring tear it would represent another slight on the £30.75m striker not to be selected ahead of or alongside Owen, Federico Macheda or Mame Biram Diouf.
The 30-year-old has started United's last two matches, the draw at the Britannia Stadium and the Carling Cup win at Leeds United, and perhaps that explained Ferguson's irritation when pressed on Berbatov's contribution to the Champions League campaign. "Of course he's got a part to play. He's one of our squad members and they've all got a part to play," the United manager said. "There are a lot of games in the Premier League, Champions League, FA Cup and Carling Cup. It's an exhausting season unless you use your squad."
The Guardian

'Mapro' 20 Morocco kuivaa Taifa Stars

RABAT, Morocco
Marouane Chamakh
KOCHA wa Morocco, Eric Gerets ametangaza kikosi cha wachezaji zaidi ya 20 wanaocheza soka ya kulipwa kona mbalimbali za dunia kwa ajili ya pambano dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars litakalofanyika Oktoba 9 kwenye mji wa Marrakech, Morocco.

Wachezaji walioitwa ni Ismail Aissati (Ajax, Uholanzi), Ahmed Ajedou (Wydad Casablanca), Jamal Alioui (Al Kharityath, Qatar), Nordin Amrabat (Kayserispor. Uturuki), Ossama Assaidi (Heerenveen, Uholanzi), Aissam Badda (FUS Rabat) na Micahael Basser wa Buraspor ya Uturuki.

Wengine ni Younes Belhanda (Montpellier, Ufaransa), Mohamed Berrabeh (Wydad Casablanca), Mbark Boussoufa (Anzhi Makhachkala, Russia), Rachid Bourabia (Mons, Belgium), Kamal Chafni (Auxerre, Ufaransa) na Marouane Chamakh wa Arsenal ya England.

Pia wamo Mohammed Chihani (Al Arabi, Qatar), Adil Chihi (Cologne, Ujerumani), Nabil Dirar (Club Brugge, Ubelgiji), Larim El Ahmadi Aroussi (Feyenoord, Uholanzi), Youssef El Arabi (Al Hilal, Saudi Arabia), Mounir El Hamdaoui (Ajax, Uholanzi) na Mostapha El Kabir wa Cagliari ya Italia.

Wachezaji wengine ni Badr El Kaddouri (Celtic, Scotland), Abdelhamid El Kaoutari (Montpellier, Ufaransa) Ayoub El Khaliqi (Wydad Casablanca), Mehdi El Moutaqui (Udinese, Italia) Youssouf Hadji (Rennes, Ufaransa) na Houssine Kharja wa Fiorentina ya Italia.

Wengine waliotajwa ni Oussama Laghrib (FUS Rabat), Nadir Lamyaghri (Wydad Casablanca), Ahmed Mohamadina (Olympic Khouribga), Mustapha Mrani (MAS), Youssef Rabeh (Wydad Casablanca), Fatah Said (Wydad Casablanca), Rachid Soulaimani (Raja Casablanca) na Adel Taarabt wa Queen Park Rangers ya England.

Kocha Misri aihofia Gabon

Wachezaji wa timu ya vijana ya Misri wakishangilia ushindi.

CAIRO, Misri

 KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Hani Ramzy amesema anatafuta njia za kidiplomasia kuhakikisha timu yake ya vijana inacheza Michezo ya Olimpiki kama ilivyokuwa mwaka 1992.
Timu yake imepangwa na Gabon, Ivory Coast na Afrika Kusini katika Kundi A.
Pia alisema haifahamu sana Gabon.
"Tumemwambia balozi wetu aliyeko Gabon kutupatia DVD za mechi za timu ya Gabon," alisema.
"Gabon ni ngumu kupata taarifa zake na mechi zake kwa kuwa haichezi sana, lakini tunahangaika kupata maelezo ya mechi kwa jumla."
Alisema pia kuwa atatumia njia kama hizo kupata taarifa za wapinzani wake wengine kabla ya mechi hizo kuanza Novemba 26 hadi Desemba 10.
Lakini licha ya kuifahamu kiasi Gabon, anaamini kuwa Misri itakuwa moja ya timu zitakazotoa upinzani mkali.
"Tunacheza na Gabon katika mechi ya kwanza, ni muhimu kwetu- naamini itakuwa mechi ngumu," aliiambia BBC Sport.

Neymar awagawa Real Madrid

WANACHAMA na mashabiki wa Real Madrid  wamegawanyika juu ya suala la kumsajili mshambuliaji wa Santos, Neymar katika dirisha dogo mwakani.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa ametawala vyombo vya habari duniani, amekuwa akiwaniwa na klabu kubwa ikiwemo Chelsea, AC Milan na Real Madrid.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amewaambia watu wake kuwa wasiangalie majina makubwa katika dirisha dogo la usajili baadaye Januari na kuangalia aina ya mchezaji.
Naye mmoja wa wanachama wa Real, Alfredo Claudio del Rey anasema: "Inatakiwa kununua wachezaji waliopo na wanaocheza vizuri, lakini si kununua wachezaji wa magazetini."
Katika mkutano huo, kulikuwa na kelele za kupinga kuja kwa mchezaji huyo nyota wa Brazil anayewaniwa na klabu mbalimbali za Ulaya. "Hatumtaki...hatumtaki Neymar...."
Neymar kwa sasa anakipiga katika klabu ya Santos inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil.

Fergie: Chezeni kama Barcelona

Wachezaji wa Manchester United wakijifua
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewataka wachezaji wake kucheza soka kama ilivyo Barcelona msimu huu.
Pamoja na timu yake kufanya vizuri katika Ligi Kuu, alimwambia Darren Fletcher, 27, kuwa huenda wakakutana na Barcelona mbele ya safari katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo wanatakiwa kujipanga mapema.
Anasema: "Kocha anasema Barcelona ni klabu inayotisha kwa kila mmoja Ulaya. na kama tunataka kushinda, ni uamuzi wetu kuanza kujipanga sasa."

Taarifa za soka Tanzania kutoka TFF

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Septemba 25, 2011
 
LESENI KWA KLABU ZA VPL
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zimekumbushwa kutekeleza kikamilifu makubaliano ya Azimio la Bagamoyo (Bagamoyo Declaration) katika semina iliyofanyika mwaka 2007 mjini Bagamoyo kati yao na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
 

Afisa Habari TFF, Boniface Wambura.

Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana Septemba 24 mwaka huu imesisitiza utekezaji wa azimio hilo ambalo lilifanyiwa tathmini ya kwanza chini ya FIFA Februari mwaka huu katika semina nyingine iliyofanyika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam kwani ni moja ya masharti ya kupata leseni kwa klabu za Ligi Kuu.
 
Pia Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Ramadhan Nassib imependekeza utekelezaji wa azimio hilo uanzie kwa klabu za Ligi Daraja la Kwanza ili kuziweka katika mazingiza mazuri ya utendaji zinapoingia Ligi Kuu.
 
Masuala ambayo yanatakiwa kutekelezwa na klabu hizo kwa mujibu wa Azimio la Bagamoyo ni kuwa na Katiba inayozingatia Katiba mfano (standard statute) iliyotolewa na TFF, kuajiri Sekretarieti kwa kuzingatia sifa za kitaaluma, kuwasilisha hesabu za fedha zilizokaguliwa kila mwaka kuanzia msimu wa 2010/2011.
 
Klabu kutenganisha majukumu ya kamati ya utendaji na Sekretarieti, benchi za ufundi kuongozwa na watu wenye sifa kwa mujibu wa kanuni za TFF (kocha na daktari wa tiba ya michezo), kuwa na timu za vijana hatua kwa hatua (U14, U17 na U20) na ofisi za kudumu (physical address).
 
Vilevile kuwa na uwanja wa kudumu wa mazoezi (kwa kuumiliki au wa kukodi kwa muda mrefu), vifaa vya kutosha vya mazoezi (kits, equipment na gym) na vifaa vya tiba ya michezo.
 
Kamati ya Mashindano imeweka msisitizo katika hilo kwa vile TFF iko mbioni kuhakikisha timu zote zinazocheza Ligi Kuu zinakuwa na leseni kwanza baada ya kutimiza masharti hayo. Kwa mantiki hiyo kupanda daraja kutokuwa sifa pekee ya kucheza Ligi Kuu.
 
Hatua hiyo pia imelenga kuziweka tayari klabu za Tanzania Bara ambazo timu zake zitashiriki michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).  CAF imesema kuanzia msimu wa 2012/2013 ni klabu zenye leseni yake tu ndizo zitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
 
VIINGILIO YANGA vs COASTAL UNION
Pambano namba 51 la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Coastal Union litachezwa Septemba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
 
Viingilio vilivyopangwa katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa. VIP C ni sh. 7,000, VIP B ni sh. 10,000 na VIP A itakuwa sh. 15,000.
 
SHOOTING YAPIGWA FAINI SH. 500,000
Kamati ya Mashindano ya TFF imeipiga faini ya sh. 500,000 timu ya Ruvu Shooting ya Mkoa wa Pwani baada ya kupata kadi sita kwenye mechi namba 40 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Septemba 17 mwaka huu Uwanja wa Mlandizi.
 
Kwa mujibu wa Kanuni namba 25 (1)(d) ya Ligi Kuu ya Vodacom, timu ambayo wachezaji wake wataoneshwa zaidi ya kadi tano katika mechi moja itatozwa faini ya sh. 500,000.
 
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari


 

Mshindi Tuzo ya Nobel Kenya afariki

NAIROBI, Kenya
MSHINDI wa Tuzo ya Nobel ya Mazingira Kenya, Wangari Maathai, amefariki hapa Kenya
akiwa na miaka 71, familia ya marehemu ilisema.
"Ni masikitiko na majonzi kuwa familia ya Prof. Wangari Maathai inatangaza msiba wa
Mwanaharakati wa Mazingira, kifo kilichotokea  jana Jumapili Nairobi Hospital kutokana na
kusumbuliwa na kansa ya mifupa," ilisema taarifa hiyo kupitia Taasisi ya Green Belt
Movement aliyoianzisha.
Maathai alikuwa mmoja wa watu mashuhuri Kenya tangu 1977, na alikuwa mpigania
ukombozi wa amani na mazingira.
Alitwaa Tuzo ya Nobel 2004 kwa kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa mazingira bora
Kenya -- ni mwanamke wa kwanza Kenyakupata heshima hiyo ya juu. Taasisi yake ilipanda
miti zaidi ya 40mil kuzunguka Afrika. Mwanamke wa Kwanza ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati kupata Shahada ya Uzamivu, PhD. Maathai pia aliwahi kuongoza Chama cha Msalaba
Mwekundu Kenya 1970.

Msimamo England baada ya mechi za mwishoni mwa wiki

P W D L GD PTS
Man Utd65101716
Man City65101416
Chelsea6411513
Newcastle6330412
Liverpool6312010
Tottenham530209
Stoke6231-29
Aston Villa615028
QPR6222-28
Everton521207
Wolves6213-37
Arsenal6213-57
Sunderland512225
Norwich5122-25
Wigan6123-45
Swansea6123-55
Fulham6042-34
Blackburn6114-54
West Brom6114-54
Bolton6105-83

Lionel Messi apiga 'hat-trick' 12


BARCELONA, Hispania
KIUNGO mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi huenda akavunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Barcelona baada ya kufikisha hat-trick 12 kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Hispania zilizompaisha kufikisha mabao 192.
Messi aliyekuwa na hat-trick 11, aliongeza nyingine wakati timu yake iliposhinda mabao 5-0 dhidi ya Atletico Madrid na sasa yuko nyuma ya mshambuliaji wa Hungary, Laszlo Kubala ambaye alifunga mabao 194 akiwa Camp Nou mwaka 1950.
Akifanikiwa kumpita, bado atakuwa na kazi ya kufikisha mabao 235, ya Cesar Rodriguez aliyoifungia klabu hiyo kati ya  1939 na 1955, na anaweza kufanya hivyo
"Nafurahia hilo. Nacheza kwa mipango, na ni wazi nafurahia kuwa mfungaji bora wa klabu," Messi anaiambia  fcbarcelona.com.
"Miaka mingi imerpita lakini bado ni (Kubala). Ninaimani nitampita. Nataka kuweka rekodi hapa".
Atletico ni timu pekee aliyoifunga mabao 14 ikiwemo hat-trick tatu.

Mtifuano Ligi ya Mabingwa Ulaya

Jumanne Sept. 27, 2011
CSKA Moscow v Inter Milan
Bayern Munich v Man City
Lyon  v Dinamo Zagreb
Man Utd  v Basle
Napoli  v Villarreal
Real Madrid v Ajax
SC Otelul Galati v Benfica
Trabzonspor v Lille

Jumatano Sept. 28, 2011
Zenit St Petersburg v FC Porto
AC Milan  v Plzen
Arsenal  v Olympiakos
BATE Borisov v Barcelona
Bayer Leverkusen v Genk
Marseille  v Borussia Dortmund
Shakhtar Donetsk v Apoel Nicosia
Valencia  v Chelsea

Lampard kuondoka Chelsea?


Andre Villas-Boas na Lampard. Picha ya REUTERS

LONDON, England
KITENDO cha kocha wa Chelsea, Andre Villas-Boas kumwacha katika benchi, Frank Lampard kimemkera mchezaji huyo mkongwe wa timu hiyo na anasema huenda akatimka.
Kiungo huyo aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Swansea City iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea ilishinda mabao 4-1.
Gazeti la Uingereza la Mail la Jumapili liliripoti kuwa aliachwa katika kikosi cha kwanza na Villas-Boas, huku akimchezesha 'dogo' Josh McEachran ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Raul Meireles ikiwa zimesalia dakika saba mpira kumalizika.
Baada ya kuwepo hali hiyo, Lampard alikuwa amejiinamia kwenye benchi, na kocha wake hakumuuliza chochote wala hakutaka kusema lolote juu ya hili.
"...Hilo sifahamu, lakini hakuna sababu ya kuzungumzia uzushi," anasema Villas-Boas.

Saturday, 24 September 2011

Maradona amtandika shabiki Arabuni

Dubai, United Arab Emirates
DIEGO Maradona, mshambuliaji wa zamani wa Argentina aliomba radhi baada ya kumpiga shabiki wa soka.
Maradona, ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Al Wasl ya United Arab Emirates, alimpiga shabiki aliyeingilia picha ambayo yeye Maradona aliyokuwa anapiga ya kutengeneza bango la kumsaidia mjukuu wake.
Maradona anasema “Nilipatwa na mshtuko wa mjukuu wangu aliyeko Argentina...lakini naomba radhi kwa kitendo nilichofanya."

Friday, 23 September 2011

Kocha Msumbiji aambiwa: Sasa basi

Maputo, Msumbiji
KOCHA wa Msumbiji, Mart Nooij amerudi nyumbani kwao, Uholanzi ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza mkataba wake.
Kocha huyo aliyeingia mkataba na Shirikisho la Soka Msumbiji (FMF) alikuwa na kazi
kubwa ya kuivusha timu ya taifa ya Msumbiji, Mambas kwa Fainali za Afrika, 2012.
Hata hivyo, timu hiyo iliyoko Kundi C, haina nafasi ya kufuzu baada ya kuchapwa bao
1-0 na Libya katika mechi ya mwisho.
"Baada ya Libya, nafahamu kuwa mambo yamemalizika," Nooij aliiambia BBC Sport.
"Nafurahia mafanikio ya Msumbiji, na nitakwenda kama rafiki."
Katika maisha yake ya soka Msumbiji akiwa na Mambas aliisaidia timu hiyo kucheza
fainali za Afrika 2010 kwa mara ya nne tangu 1998. Kocha wa zamani wa Angola, David
Nascimento ndiye aliyechukua nafasi yake.

Mtihani mwingine kwa kocha wa Arsenal

LONDON, England
KIVUMBI cha Ligi Kuu kinaendelea leo kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kurudisha imani kwa mashabiki wake wakati timu yake itakaporudi nyumbani, Emirates kucheza na Bolton.
Wenger ambaye timu yake ilifungwa mabao 4-3 na Blackburn wikiend iliyopita, atakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha timu yake inashinda mechi ya leo.
Pamoja na kuanza vibaya msimu huu ikiwa ni miaka 58, Wenger anasema timu yake iko vizuri na itashinda mchezo wa leo licha ya kusema ana wasiwasi.
"Naweza kushinda lakini nina wasiwasi," anasema Wenger, ambaye timu yake iko nyuma ya Manchester United kwa pointi 11. Arsenal iko nafasi ya 17 ikiwa na pointi nne na ingekuwa na pointi 15. Kwa, United imeshinda mechi tano ikiwemo ya Chelsea, na Arsenal, iko kileleni.

Mechi za Jumamosi Sept. 24;
Chelsea v Swansea
Liverpool v Wolves
Man City v Everton
Newcastle v Blackburn
Stoke v Man Utd
West Brom v Fulham
Wigan v Tottenham

IOC chief demands 2012 boxing bribe evidence from BBC

International Olympic Committee president Jacques Rogge has called on the BBC to provide evidence into claims attempts have been made to fix boxing results at the 2012 Olympic Games.
BBC Newsnight uncovered evidence of secret payments from Azerbaijan to World Series Boxing, to allegedly guarantee two golds.
"We take every allegation very seriously," said Rogge.
The International Amateur Boxing Association denies the claim.
AIBA is the international governing body for the sport of boxing recognised by the International Olympic Committee (IOC), while World Series Boxing, a franchised league of professional boxing, is one of its initiatives.
AIBA is, however, investigating the claims and Rogge added: "We welcome the inquiry by the AIBA and we have asked the BBC to provide evidence."