Monday, 26 September 2011

Mshindi Tuzo ya Nobel Kenya afariki

NAIROBI, Kenya
MSHINDI wa Tuzo ya Nobel ya Mazingira Kenya, Wangari Maathai, amefariki hapa Kenya
akiwa na miaka 71, familia ya marehemu ilisema.
"Ni masikitiko na majonzi kuwa familia ya Prof. Wangari Maathai inatangaza msiba wa
Mwanaharakati wa Mazingira, kifo kilichotokea  jana Jumapili Nairobi Hospital kutokana na
kusumbuliwa na kansa ya mifupa," ilisema taarifa hiyo kupitia Taasisi ya Green Belt
Movement aliyoianzisha.
Maathai alikuwa mmoja wa watu mashuhuri Kenya tangu 1977, na alikuwa mpigania
ukombozi wa amani na mazingira.
Alitwaa Tuzo ya Nobel 2004 kwa kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa mazingira bora
Kenya -- ni mwanamke wa kwanza Kenyakupata heshima hiyo ya juu. Taasisi yake ilipanda
miti zaidi ya 40mil kuzunguka Afrika. Mwanamke wa Kwanza ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati kupata Shahada ya Uzamivu, PhD. Maathai pia aliwahi kuongoza Chama cha Msalaba
Mwekundu Kenya 1970.

No comments:

Post a Comment