Monday, 26 September 2011

Lampard kuondoka Chelsea?


Andre Villas-Boas na Lampard. Picha ya REUTERS

LONDON, England
KITENDO cha kocha wa Chelsea, Andre Villas-Boas kumwacha katika benchi, Frank Lampard kimemkera mchezaji huyo mkongwe wa timu hiyo na anasema huenda akatimka.
Kiungo huyo aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Swansea City iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Chelsea ilishinda mabao 4-1.
Gazeti la Uingereza la Mail la Jumapili liliripoti kuwa aliachwa katika kikosi cha kwanza na Villas-Boas, huku akimchezesha 'dogo' Josh McEachran ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Raul Meireles ikiwa zimesalia dakika saba mpira kumalizika.
Baada ya kuwepo hali hiyo, Lampard alikuwa amejiinamia kwenye benchi, na kocha wake hakumuuliza chochote wala hakutaka kusema lolote juu ya hili.
"...Hilo sifahamu, lakini hakuna sababu ya kuzungumzia uzushi," anasema Villas-Boas.

No comments:

Post a Comment