![]() |
C. Ronaldo, Real Madrid |
Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaingia hatua nyingine leo, baada ya timu kadhaa kufanya vema katika mechi za ufunguzi.
Manchester United, Manchester City na Inter Milan zina kazi ngumu leo kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Manchester United, Manchester City na Inter Milan zina kazi ngumu leo kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Kila mmoja anatambua kuwa hakuna timu iliyotwaa ubingwa mara mbili tangu kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, kila mmoja anaangalia jinsi gani ya kuivua ubingwa Barcelona.
Klabu hiyo ya Catalan itataka kujiimarisha zaidi kwani yenyewe na United zilitoka sare. Man United ilitoka sare na Benfica, City ilifanya hivyo kwa Napoli lakini Inter ilishangaza wengi kwa kuchapwa na Trabzonspor ikiwa nyumbani.
City, na United ambazo ziko kileleni mwa Ligi Kuu ya England, ilicheza na Napoli, na kuwalazimisha sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Etihad na kumwacha kocha, Roberto Mancini akijisifu "Nilichanganyikiwa kwa sababu ilikuwa mechi ya kwanza".
Mechi za leo
Bayern itakuwa na kazi ya kupunguza makali ya washambuliaji wa City wanaojengwa na Tevez, Balotelli, Owen Hargreaves na Yaya Toure.
Bayern itakuwa na kazi ya kupunguza makali ya washambuliaji wa City wanaojengwa na Tevez, Balotelli, Owen Hargreaves na Yaya Toure.
![]() |
W. Rooney, Man United |
Hata hivyo, Bayern inajivunia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Villarreal na ushindi wake leo utaisaidia kujiweka katika nafasi nzuri zaidi.
Nayo Manchester United, kwa upande wake itakuwa na kibarua cha vijana wa Uswisi; Basel lakini watamkosa, Wayne Rooney.
Kocha wa United; Sir Alex Ferguson ameanza kuingia hofu kukosekana kwa Rooney, huku akiendelea kusikilizia maumivu ya Javier Hernandez aliyeumia katika mechi waliyotoka sare ya 1-1 na Stoke.
Naye kocha wa Basel, Thorsten Fink anasema ana kila sababu ya kuisimamisha United, kama alivyofanya kwa Bayern Munich ilipofungwa 1999 na Red Devils mechi ya Barcelona.
Inter ambayo ilianza vibaya ligi hiyo na baada ya kumtimua kocha wake, Giun Piero Gasperini na wamemnasa kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus, Claudio Ranieri.
Ranieri alishinda mechi ya kwanza 3-1 dhidi ya Bologna Jumamosi, lakini Wesley Sneijder, beki wa Brazil, Maicon na kiungo wa Serbia, Dejan Stankovic watakosa mechi ya Kundi B, itakutana na CSKA mjini Moscow.
Katika kundi hilo, mabingwa wa Ufaransa, Lille itakutana na Trabzonspor wakati Lyon itacheza na Dinamo Zagreb, na Real Madrid itakuwa nyumbani kuivaa Ajax.
No comments:
Post a Comment