![]() |
Adebayor kushoto. PHOTO/Getty. |
LONDON, England
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, ambaye aliingia kipindi cha pili katika mechi dhidi ya Wigan alicheza huku akiwa haoni jicho moja baadaya kugongana na mchezaji wa upinzani, lakini akasema anataka kuwa fiti ili aweze kufunga bao la kwanza dhidi ya Arsenal kufuta bao lile alilolaumiwa kwa kushangilia sana dhidi ya Arsenal alipokuwa akiitumikia Manchester City miaka miwili iliyopita."Sikuwa nauona mpira. Sikuwa naona mtu anayekuja," anasema Adebayor, ambaye hata hivyo, alicheza mechi hiyo hadi mwisho. "Lakini nzuri zaidi, nilikuwa na jicho moja, lakini tuliondoka na pointi tatu.Kipindi cha kwanza nilicheza vizuri kwa sababu nilikuwa naona kwa macho yote."
No comments:
Post a Comment