Monday, 26 September 2011

Fergie: Chezeni kama Barcelona

Wachezaji wa Manchester United wakijifua
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewataka wachezaji wake kucheza soka kama ilivyo Barcelona msimu huu.
Pamoja na timu yake kufanya vizuri katika Ligi Kuu, alimwambia Darren Fletcher, 27, kuwa huenda wakakutana na Barcelona mbele ya safari katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo wanatakiwa kujipanga mapema.
Anasema: "Kocha anasema Barcelona ni klabu inayotisha kwa kila mmoja Ulaya. na kama tunataka kushinda, ni uamuzi wetu kuanza kujipanga sasa."

No comments:

Post a Comment