WANACHAMA na mashabiki wa Real Madrid wamegawanyika juu ya suala la kumsajili mshambuliaji wa Santos, Neymar katika dirisha dogo mwakani.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa ametawala vyombo vya habari duniani, amekuwa akiwaniwa na klabu kubwa ikiwemo Chelsea, AC Milan na Real Madrid.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amewaambia watu wake kuwa wasiangalie majina makubwa katika dirisha dogo la usajili baadaye Januari na kuangalia aina ya mchezaji.
Naye mmoja wa wanachama wa Real, Alfredo Claudio del Rey anasema: "Inatakiwa kununua wachezaji waliopo na wanaocheza vizuri, lakini si kununua wachezaji wa magazetini."
Katika mkutano huo, kulikuwa na kelele za kupinga kuja kwa mchezaji huyo nyota wa Brazil anayewaniwa na klabu mbalimbali za Ulaya. "Hatumtaki...hatumtaki Neymar...."
Neymar kwa sasa anakipiga katika klabu ya Santos inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil.

No comments:
Post a Comment