Monday, 26 September 2011

Lionel Messi apiga 'hat-trick' 12


BARCELONA, Hispania
KIUNGO mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi huenda akavunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Barcelona baada ya kufikisha hat-trick 12 kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Hispania zilizompaisha kufikisha mabao 192.
Messi aliyekuwa na hat-trick 11, aliongeza nyingine wakati timu yake iliposhinda mabao 5-0 dhidi ya Atletico Madrid na sasa yuko nyuma ya mshambuliaji wa Hungary, Laszlo Kubala ambaye alifunga mabao 194 akiwa Camp Nou mwaka 1950.
Akifanikiwa kumpita, bado atakuwa na kazi ya kufikisha mabao 235, ya Cesar Rodriguez aliyoifungia klabu hiyo kati ya  1939 na 1955, na anaweza kufanya hivyo
"Nafurahia hilo. Nacheza kwa mipango, na ni wazi nafurahia kuwa mfungaji bora wa klabu," Messi anaiambia  fcbarcelona.com.
"Miaka mingi imerpita lakini bado ni (Kubala). Ninaimani nitampita. Nataka kuweka rekodi hapa".
Atletico ni timu pekee aliyoifunga mabao 14 ikiwemo hat-trick tatu.

No comments:

Post a Comment