Friday, 23 September 2011

Kocha Msumbiji aambiwa: Sasa basi

Maputo, Msumbiji
KOCHA wa Msumbiji, Mart Nooij amerudi nyumbani kwao, Uholanzi ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza mkataba wake.
Kocha huyo aliyeingia mkataba na Shirikisho la Soka Msumbiji (FMF) alikuwa na kazi
kubwa ya kuivusha timu ya taifa ya Msumbiji, Mambas kwa Fainali za Afrika, 2012.
Hata hivyo, timu hiyo iliyoko Kundi C, haina nafasi ya kufuzu baada ya kuchapwa bao
1-0 na Libya katika mechi ya mwisho.
"Baada ya Libya, nafahamu kuwa mambo yamemalizika," Nooij aliiambia BBC Sport.
"Nafurahia mafanikio ya Msumbiji, na nitakwenda kama rafiki."
Katika maisha yake ya soka Msumbiji akiwa na Mambas aliisaidia timu hiyo kucheza
fainali za Afrika 2010 kwa mara ya nne tangu 1998. Kocha wa zamani wa Angola, David
Nascimento ndiye aliyechukua nafasi yake.

No comments:

Post a Comment