![]() |
Carlos Tevez akiitumikia klabu yake. |
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema anataka kuona Carlos Tevez "anajiondoa mwenyewe klabuni" baada ya kugoma kuingia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich.
Mancini alimtaka mchezaji huyo kuingia dakika 35 wakati timu yake ilipokuwa nyuma kwa mabao 2-0.
Mancini alisema: "Kama mimi ni kocha hapa, sitaki kumuona. Ameshamalizana na mimi.
"Kama tunataka kuimarisha timu, kwa mtu kama Carlos hatufai. Kwangu tumemalizana."
No comments:
Post a Comment