Monday, 26 September 2011

'Mapro' 20 Morocco kuivaa Taifa Stars

RABAT, Morocco
Marouane Chamakh
KOCHA wa Morocco, Eric Gerets ametangaza kikosi cha wachezaji zaidi ya 20 wanaocheza soka ya kulipwa kona mbalimbali za dunia kwa ajili ya pambano dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars litakalofanyika Oktoba 9 kwenye mji wa Marrakech, Morocco.

Wachezaji walioitwa ni Ismail Aissati (Ajax, Uholanzi), Ahmed Ajedou (Wydad Casablanca), Jamal Alioui (Al Kharityath, Qatar), Nordin Amrabat (Kayserispor. Uturuki), Ossama Assaidi (Heerenveen, Uholanzi), Aissam Badda (FUS Rabat) na Micahael Basser wa Buraspor ya Uturuki.

Wengine ni Younes Belhanda (Montpellier, Ufaransa), Mohamed Berrabeh (Wydad Casablanca), Mbark Boussoufa (Anzhi Makhachkala, Russia), Rachid Bourabia (Mons, Belgium), Kamal Chafni (Auxerre, Ufaransa) na Marouane Chamakh wa Arsenal ya England.

Pia wamo Mohammed Chihani (Al Arabi, Qatar), Adil Chihi (Cologne, Ujerumani), Nabil Dirar (Club Brugge, Ubelgiji), Larim El Ahmadi Aroussi (Feyenoord, Uholanzi), Youssef El Arabi (Al Hilal, Saudi Arabia), Mounir El Hamdaoui (Ajax, Uholanzi) na Mostapha El Kabir wa Cagliari ya Italia.

Wachezaji wengine ni Badr El Kaddouri (Celtic, Scotland), Abdelhamid El Kaoutari (Montpellier, Ufaransa) Ayoub El Khaliqi (Wydad Casablanca), Mehdi El Moutaqui (Udinese, Italia) Youssouf Hadji (Rennes, Ufaransa) na Houssine Kharja wa Fiorentina ya Italia.

Wengine waliotajwa ni Oussama Laghrib (FUS Rabat), Nadir Lamyaghri (Wydad Casablanca), Ahmed Mohamadina (Olympic Khouribga), Mustapha Mrani (MAS), Youssef Rabeh (Wydad Casablanca), Fatah Said (Wydad Casablanca), Rachid Soulaimani (Raja Casablanca) na Adel Taarabt wa Queen Park Rangers ya England.

No comments:

Post a Comment