
United walionekana kuridhika na mabao mawili ya kipindi cha kwanza ya Danny Welbeck, lakini Basel ilisawazisha kabla ya Fabian Frei kufunga la tatu baada ya mabao ya Alexander Frei.
Wakati ndugu zao wakisalimika, Manchester City walitandikwa mabao 2-0 na Bayern Munich huku Mario Gomez akifunga mabao yote mawili katika mechi hiyo ya Kundi A na kuifanya Bayern kuwa na pointi sita katika mechi mbili.
Real Madrid, kwa upande wake, ilikuwa ikisaka rekodi ya taji la 10 la Ulaya kwa kujipatia pointi sita katika mechi ya Kundi D baada ya kuizabua 3-0 Ajax Amsterdam kwa mabao ya Cristiano Ronaldo, Kaka na Karim Benzema.
Inter Milan iliyokuwa nyuma kwa mabao 2-0 mbele ya CSKA Moscow iliibuka na kushinda mabao 3-2 baada ya kazi nzuri ya Mauro Zarate aliyefunga bao la ushindi na kufanya kikosi cha kocha, Claudio Ranieri kuendelea kujipa matumaini ya kufanya vizuri.
Mechi nyingine, Napoli iliifunga Villarreal 2-0 mechi ya Kundi A, Trabzonspor ikatoka sare ya 1-1 na Lille ikiwa ni mechi ya Kundi B wakati Benfica iliifunga Otelul Galati 1-0 katika Kundi C. Nayo Olympique Lyon ikailaza Dinamo Zagreb 2-0 katika mpambano wa Kundi D.
Mechi za Makundi E-H zinazochezwa leo Jumatano Sept. 28, 2011
Zenit St Petersburg v FC Porto
AC Milan v Plzen
Arsenal v Olympiakos
BATE Borisov v Barcelona
Bayer Leverkusen v Genk
Marseille v Borussia Dortmund
Shakhtar Donetsk v Apoel Nicosia
Valencia v Chelsea
No comments:
Post a Comment