Monday, 26 September 2011

Kocha Misri aihofia Gabon

Wachezaji wa timu ya vijana ya Misri wakishangilia ushindi.

CAIRO, Misri

 KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Hani Ramzy amesema anatafuta njia za kidiplomasia kuhakikisha timu yake ya vijana inacheza Michezo ya Olimpiki kama ilivyokuwa mwaka 1992.
Timu yake imepangwa na Gabon, Ivory Coast na Afrika Kusini katika Kundi A.
Pia alisema haifahamu sana Gabon.
"Tumemwambia balozi wetu aliyeko Gabon kutupatia DVD za mechi za timu ya Gabon," alisema.
"Gabon ni ngumu kupata taarifa zake na mechi zake kwa kuwa haichezi sana, lakini tunahangaika kupata maelezo ya mechi kwa jumla."
Alisema pia kuwa atatumia njia kama hizo kupata taarifa za wapinzani wake wengine kabla ya mechi hizo kuanza Novemba 26 hadi Desemba 10.
Lakini licha ya kuifahamu kiasi Gabon, anaamini kuwa Misri itakuwa moja ya timu zitakazotoa upinzani mkali.
"Tunacheza na Gabon katika mechi ya kwanza, ni muhimu kwetu- naamini itakuwa mechi ngumu," aliiambia BBC Sport.

No comments:

Post a Comment